Wataka kampeni ya ‘Baki Magufuli’ ipigwe ‘stop’

Serikali imeombwa kukomesha kampeni mbalimbali zinazoanzishwa ikiwamo ya 'Baki Magufuli' ili kuondoa sintofahamu iliyopo kwamba wenye kampeni hizo wanatumwa na Rais John Magufuli.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Agosti 3 na Shirika Lisilo la Kiserikali la Vijana na Wanawake (Tafeyoco) wakati wakizungumza na wanahabari kuhusu hali ya utawala bora na demokrasia inayoendelea nchini.

Mwenyekiti wa Tafeyoco, Elvice Makumbo amesema kampeni hizo siyo muda wake kwa sasa kwani zinatachochea kuzalisha kwa kampeni nyingine hali itakayoleta mvurugano nchini.

"Tukiwaacha hawa wenye kampeni ya 'Baki Magufuli' watazaliwa wengine wenye kampeni ya 'Ondoa Magufuli' madarakani na wao watataka kuisambaza kampeni yao," amesema Makumbo.

Makumbo amesema ni wakati muafaka kwa Serikali kupiga marufuku kampeni hizo, kwani Tanzania inaongozwa kwa Katiba inayoeleza awamu ya kwanza ya rais ni vipindi vitano baada ya hapo uchaguzi mkuu mwingine unaitishwa.

Amesema Rais Magufuli anafanya kazi kubwa kuiongoza nchi na kwamba haitaji ‘tochi’ kupima uwezo wake hivyo kuanzisha kampeni za yeye kubaki ni kutengeneza chuki kati yake na Watanzania ambao wanaikubali kazi yake.

Mbali na hilo, Makumbo amewataka viongozi wa vyama siasa nchini kuacha tabia ya kuwatumia vijana kuendeleza siasa katika mitandao ya kijamii, kwani baadhi ya vijana wanatumia nafasi hiyo kuandika habari za uchochezi dhidi ya Serikali.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com