Shilingi milioni 860,000,000 Kutumika Kuzima Mwenge wa Uhuru Mwaka huu

NA Khamis Malik, WKUWVWW
WIZARA ya Kazi, Uwezshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto imeridhishwa na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Mkoa wa Mjini Magharibi juu ya maandalizi ya kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru kinachotarajiwa kufanyika Oktoba 14 mwaka huu katika kiwanja cha Amaan mijini hapa.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya Mkoa wa Mjini Magharibi katika kikao cha pamoja cha Uongozi wa Wizara hiyo na Mkoa huo huko ofisini Mwanakwerekwe, Mwenyekiti wa kikao hicho, Moudline Castico, alisema  kamati ya maandalizi inaendelea kufanya kazi nzuri na kuhimiza shughuli zilizobakia kukamilishwa kwa wakati ili kufanikisha ipasavyo kilele cha mbio za mwenge Kitaifa mwaka huu.
Alisema  kufanikisha kilele hicho ni lazima kwa vile Mkoa huo umepewa heshima kubwa na taifa ya kuwa mwenyeji wa shughuli hiyo muhimu ambayo itakwenda sambamba na kilele cha maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa na kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Alifahamisha kuwa pamoja na kupokea taarifa ya maandalizi kikao hicho pia kimepokea taarifa ya makisio na makadirio ya matumizi kwa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na makabidhiano katika viwanja vya ndege Kisauni, Unguja na Vitongoji, Pemba.
Waziri Moudline aliwaomba wajumbe wa mkutano huo kuendeleza mashirikiano zaidi kati yao na Serikali zote mbili za Muungano Tanzania na Mapinduzi Zanzibar pamoja na kumshukuru Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Watoto, Tanzania, Jenesta Muhagama  kwa kuleta kuwakilisha katika kikao hicho.
Mapema akiwasilisha taarifa ya Mkoa wa Mjini Magharibi juu ya Maandalizi hayo, Mkuu wa Mkoa huo, Ayoub Mohammed Mahmoud alisema Serikali ya Mkoa wake hadi sasa imeweza kutekeleza mambo kadhaa ikiwemo kuangalia muongozo, kuunda kamati mbili na kuandaa bajeti ya utekelezaji wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Kitaifa.
Alifahamisha kuwa kamati ya fedha tayari imeshafanya makadirio na kuridhia jumla ya shilingi milioni 860,000,000 kutumika katika shughuli hiyo na kusema kuwa kati ya idadi hiyo ya fedha mkoa umeomba milioni 560,000,000 kutoka Serikali kuu na zitakazobakia zitatolewa na Serikali yake ya Mkoa.
Mkuu huyo wa Mkoa pia alisema kamati pia imewasilisha mapendekezo ya sare itakayotumika pamoja na rasimu ya vielelezo mbali mbali vitakavyotumika katika kustawisha sherehe hizo za kilile cha Mwenge wa Uhuru Kitaifa hapa nchini.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com