Pingamizi la CUF ya Maalim Seif latupiliwa mbali na Mahakama

August 11, 2017 Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali maombi ya Bodi ya CUF inayomuunga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif ya kutaka Msajili wa Vyama vya Siasa asitoe ruzuku kwa CUF upande wa Profesa Ibrahim Lipumba.

Maombi hayo namba 21 ya mwaka 2017 yametupiliwa mbali na Jaji Wilfred Dyansobera, baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata anayemuwakilisha mdaiwa wa pili Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kusema kesi imeitishwa kwa ajili ya uamuzi.

Katika uamuzi maombi hayo ambayo mdaiwa wa kwanza ni Prof. Lipumba, Jaji Dyansobera amesema anakubaliana na moja kati ya pingamizi la AG kwamba vifungu vya sheria vilivyotumika kufungua shauri hilo sio sahihi.

Hata hivyo, amesema anakubaliana na hoja za Bodi hiyo iliyo upande wa Maalim Seif kwamba suala la Bodi hiyo kutokuwa na uhalali linahitaji ushahidi wa kina.

Aidha, kuhusu suala la Maalim Seif kusaini hati mbalimbali za shauri hilo bila kupewa mamlaka, amesema hilo sio pingamizi kwani Mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa kuangalia kiapo tu.

>>>”Hivyo mahakama imetupilia mbali maombi hayo, kwa sababu sheria iliyotumiwa kufungua maombi hayo sio sahihi, lakini waombaji wanaweza kukata rufaa ama kufungua kesi nyingine.”

Baada ya kuelezwa hayo, upande wa Maalim wamesema watafungua upya kesi hiyo


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com