Niyonzima: "Mimi ni mchezaji wa Simba rasmi tutakuta uwanjani kesho

Kiungo wa kimataifa Haruna Niyonzima ambaye kwa sasa anachezea timu ya Simba SC amesema hana maneno mengi ya kuyaongea ila mengi watayakuta uwanjani siku ya kesho katika mechi yao ya kirafiki dhidi ya Rayon FC ya Rwanda katika uwanja wa Taifa.


Kiungo Niyonzima akiwa pamoja na Afisa Habari Haji Manara.
Niyonzima amebainisha hayo wakati walipokuwa wanatambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari na Afisa mawasiliano wa Simba, Haji Manara.
"Mimi ni mchezaji wa Simba rasmi mambo mengine tutakuta uwanjani kesho zaidi", amesema Niyonzima 
Kwa upande wake Afisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara amewataka mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu wajitokeze kutazama mtanange huo ambao utakuwa wa aina yake.
"Walisema hawezi kuja sasa amekuja, kwa hiyo kesho Kocha akiamua kumpanga atamchezesha ingawa matarajio yetu makubwa atacheza yeye pamoja na wachezaji wote wageni kwa sababu ni siku maalum ya utambulisho kwa timu pamoja na jezi zetu tukazokuwa tunacheza tukiwa 'Home and Away", amesema Manara.
Kwa upande mwingine, mechi ya kesho itakuwa ya tatu kuchezwa na simba kujiandaa kuelekea michuano ya Ligi kuu huku wakiwa wamepoteza mechi moja wakifungwa na timu ya Orlando Pirate bao 1-0 na nyingine kutoka sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Bidvest FC zote wamechezea nchini Afrika ya kusini walipokuwa wameenda kuweka kambi ya maalum ya maandalizi msimu mpya.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com