Niyonzima: Hakuna kama Yanga


Kiungo wa kimataifa wa Simba ,Haruna Niyonzima ambaye jana ametambulishwa rasmi na kucheza katika mechi ya kirafiki kati ya Simba na Rayon Sports FC ya Rwanda ambapo Simba iliibuka mshindi wa goli moja amefunguka na kusema hakuna klabu kama Yanga.

Haruna Niyonzima alisema hayo jana baada ya kumaliza mchezo alipokuwa akitoa shukrani kwa mashabiki wa timu yake ya zamani na viongozi na kusema katika maisha yake ya mpira hakuna klabu ambayo amechezea kwa muda mrefu duniani zaidi ya Yanga.

"Mimi nawashukuru Yanga unajua Yanga ni timu ambayo mpaka sasa hivi nimecheza misimu mingi sana kuliko timu zote duniani ambazo nimewahi kucheza kwa hiyo ni kitu cha kuwashukuru kwani nimeishi nao vizuri, mashabiki, wanayanga na wapenzi wa Haruna ambao walikuwa wananipenda nikiwa Yanga na watu watu wote waliokuwa wanani 'support' nikiwa Yanga wamenionyesha ushirikiano lakini Mungu ndiyo hupanga mambo yake mengine nimekuja Simba naamini nimekuja kufanya kazi" alisema Haruna Niyonzima

Aidha Haruna amesema kuwa katika maisha yake hakuwahi kufikiri kucheza Yanga wala Simba kwani hakuwahi kuwa na ndoto ya kucheza mpira nchini Tanzania

"Mimi sikuwa hata na ndoto ya kucheza mpira Tanzania lakini Mungu yeye ndiye huwa anajua wapi mtu atakwenda kwa hiyo sioni tatizo saizi kuwa Simba nashukuru na kuendelea kufanya kazi na kazi mtu unafanya sehemu yoyote" alisema Haruna Niyonzima

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com