Mwenyekiti UVCCM Arusha Kufikishwa Mahakamani Kwa Kujifanya Usalama wa Taifa

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengai Sabaya ambaye ni Diwani wa Sambasha anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kughushi na kutumia kitambulisho cha Usalama wa Taifa.

Kamanda wa Polisi Arusha Charles Mkumbo amesema Sabaya anashikiliwa kwa kosa alilolitenda awali ambapo Polisi waliliondosha shauri hilo Mahakani kwa kuwa upelelezi ulikuwa haujakamilika na sasa umeshakamilika.

”Anatarajia kufikishwa Mahakamani wakati wowote. Ni kosa ambalo alilitenda huko nyuma na tuliliondosha Mahakamani kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi. Sasa uchunguzi umekamilika na hati iko timamu na atafikishwa Mahakamani.

“Kosa alilokamatwa nalo ni alijifanya Afisa wa Usalama wa Taifa kitendo ambacho si cha kweli, yeye sio Afisa wa Idara hiyo.

“Hatuwezi kumzuwia mtu kusema chochote lakini ukweli ndio huo na hili shauri halijatokea leo, lilishatokea kitambo. Ni suala tu la kitaalamu kama Wapelelezi. Kupeleleza kesi ni ili iwe na mafanikio. Kwa hiyo hilo suala la watu kusema masuala ya kisiasa sisi sio wanasiasa. Sisi ni watendaji tunaofanyakazi kwa mujibu wa sheria.”  Amesema Kamanda Charles Mkumbo.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com