Mtangazaji wa XXL ya Clouds FM afunga Ndoa Leo

Baada ya Mtangazaji wa Clouds Media Group, Babuu wa kitaa kuaga ukapela wiki iliyopita, hatimaye mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Kenedy The Remedy amefunga ndoa.
Kenedy amefunga ndoa leo jijini Dar es salaam na kuudhuriwa na watu wake wa karibu wa familia yake na familia ya bibi Harusi
Kenny anaingia katika orodha ya watu maarufu waliofunga ndoa mwaka huu ikiongozwa na Madam Flora, Mx Carter, Producer Dx, Professor Jay na Babuu wa kitaa.
Kwa niaba ya Team nzima ya eddy blog tunakupongeza kwa hatua hii muhimu katika maisha yako.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com