Msako wa nyumba kwa nyumba kuwasaka wakopaji


Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, James Ihunyo ameongoza msako wa nyumba kwa nyumba kuwasaka wakulima mia nne ambao walikopa zaidi ya milioni mia saba na tisini kwa ajili ya kuongeza uzalishaji katika sikimu ya umwagiliaji ya Mkula.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo mkoani Morogoro (TADB) kwa kushirikiana na vyombo vya dola akiwepo Mkuu wa Wilaya hiyo wamefanikiwa kuwakamata viongozi saba wa sikimu hiyo na kuwataka kufikia tarehe 25 ya mwezi huu wawe wamelipa kiasi hicho cha fedha zote wanazodaiwa.

"Hela ya mkopo ni lazima irejeshwe, kwa hatua ya mwanzo leo tumewakamata wale viongozi wote wa sikimu ambao hawajarejesha mkopo tumewapeleka polisi ili wafikishwe kwenye hatua za kisheria na kwenda mahakamani, kuna wale ambao wamekimbia baada ya kusikia tunakuja ila nasikia wapo humu humu nina uhakika serikali ina mkono mrefu najua hazitapita siku mbili wote lazima wakamatwe na nimemuelekeza kamanda wa polisi wa Wilaya ahakikishe amewakamata wote ambao wamepewa fedha za serikali wamezitumia wengine kuoa au kufanya sherehe wote wakamatwe" alisema James Ihunyo Mkuu wa Wilaya ya Kilombero

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com