Mbaroni akijaribu kuiba mtoto

NA MARYAM HASSAN
KATIKA hali isiyokua ya kawaida kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Omar Ali Haji (29), mkaazi wa Bububu amekamatwa na Jeshi la Polisi, akikabiliwa na tuhuma za kutaka kuiba mtoto katika hospitali ya Mnazimmoja.
Kijana huyo alijinasibisha kuwa mfanyakazi wa hospitali hiyo kwa njia za ghilba ambapo alimtaka mama kumpatia mtoto anaegua, daftari lake la matibabu na fedha kwa lengo la kumrahisishia upatikanaji wa tiba , lakini kinyume chake imebainika kuwa alikuwa na nia ya kutaka kutoroka na mtoto huyo.
Gazeti la zanzibarleo lilizungumza na mama wa mtoto huyo Maryam Suleiman Hamadi, ambaye alisema alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kumpeleka mtoto wake ambae anasumbuliwa na matatizo ya mkojo.
Alisema wakati yupo mapokezi alifika kijana huyo aliyejifanya daktari anayehusika na kutoa dawa katika hospitali hiyo kwa lengo la kumsaidia ili aepukane na foleni kubwa ya kusubiri dawa.
Maryam alieleza kuwa kijana huyo alimwambia kuwa kwa sasa hospitalini hapo wamefika madaktari kutoka China ambao wamekuja kwa ajili ya kutibu watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya mkojo pia wamekuja na dawa nzuri.
Alisema mara baada ya maelezo hayo alimkabidhisha mtoto kwa kijana huyo na fedha za matibabu huku akimfuata nyuma kwa sababu tayari alishaingiwa na shaka ya kuwa mwanawe hayuko katika mikono salama.
Aidha alieleza kuwa kijana huyo alipofika kwenye kona ya hospitali alimtelekeza mtoto huyo, ambapo kijana huyo alitaka kujaribu kutoroka, lakini hakufanikiwa kwa sababu aliweza kumdhibiti kwa kumtaka ampe fedha zake huku akimnadia mwizi.
“Jambo la kushukuru askari waliokuwepo katika hospitali hiyo waliweza kuufunga mlango na kumdhibiti kwa kuweza kuwa nia yake ni kutoroka ndani ya jengo hilo”, alisema kwa masikitiko.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com