LIVE Kutoka Tanga: Waziri Kalemani atangaza Leo Kukikatia Umeme Kiwanda

Serikali imetangaza kukikatia umeme leo hii kiwanda cha Rhino cha mkoani Tanga kutokana na kudaiwa bili kubwa ya umeme

Akizungumza leo mbele ya Rais John Magufuli, Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt Medadi Kalemani amesema kiwanda cha Rhino Kitakatiwa Umeme baada ya shughuli za uzinduzi wa kiwanda cha saruji cha Kilimanjaro ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais la kukata umeme kwa wale wote wanaodaiwa


Rais Magufuli yupo Mkoani Tanga na hii leo anazindua kiwanda kikubwa cha Kutengeneza saruji cha Kilimanjaro kilichopo mkoani humo, hivyo waziri Kalemani amesema kiwanda hicho hakidaiwi bili ya umeme, lakini suala la kukatikakatika kwa umeme linashughulikiwa mara moja

Bonyeza hapo chini umsikilize:-


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com