Jeshi la polisi lamtia nguvuni mwanaume aliyekuwa kavaa nguo za Kike

Jeshi la Polisi Mkoani Pwani, limemtia nguvuni kijana wa kiume mkazi wa Mbagala Jijini Dar es Salaam ambaye huvaa mavazi ya kike kama madera, hijabu na kuficha sura yake kwa kuvaa nikabu kisha kufanya matukio ya kiuhalifu.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna alisema kijana huyo (jina limehifadhiwa)amekamatwa maeneo ya picha ya ndege barabara ya kuelekea Magereza akiwa amevaa mavazi hayo.
Kamanda Shanna alieleza kwamba,wamemkamata baada ya kumwekea mtego uliowekwa na makachero waliokuwa wamepata taarifa kutoka kwa wasiri waliokuwa wanamtilia mashaka na kufanikiwa kumkamata akiwa kwenye bodaboda akielekea maeneo ya Magereza-Kibaha.
Kamanda shanna alisema “Tunaendelea kumhoji kujua ni kwanini avae mavazi ya kike na tunawashukuru wananchi na wasiri wetu kwa kuendelea kutoa ushirikiano.”
Hivi karibuni kijana huyo alisababisha taharuki kwa wakazi wa Picha ya Ndege baada ya kumuona akiwa anawasiliana na mtu mwingine huku yeye akijifanya ni mwanamke.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com