IGP Sirro: "Ukiuwa kwa upanga utaondoka kwa upanga"


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amefunguka na kuwataka wananchi wa Kibiti sasa kuishi kwa amani na wasiwe na wasiwasi wowote kwani sasa hali ni shwari kutokana na kuimaliza kwa usalama katika maeneo hayo.

IGP Sirro amesema hayo siku moja baada ya jeshi la polisi kuuwa watuhumiwa 13 wa uhalifu ambao walikuwa wakilisumbua jeshi la polisi kwa kufanya matukio mbalimbali na kujificha mkoani Pwani katika maeneo ya Kibiti.

"Ndugu zangu nilitaka kuwaambia tuko salama sana mwenye kusali aende kusali hakuna mtu yupo juu ya sheria wewe ukiuwa kwa upanga basi utaondoka kwa upanga, serikali yenu ipo makini Amiri Mjeshi Mkuu ambaye ni Rais wetu Magufuli anawapenda sana alikuwa anasikitika kuona watu hamfanyi maendeleo yenu mnaogopa hao watu wa hovyo hovyo, wamebakia wachache ila salamu wanazo tayari" alisema IGP Sirro

Aidha Sirro aliwapongeza polisi kwa kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama mkoani Pwani na maeneo jirani hali ambayo sasa imeleta utulivu katika maeneo hayo huku akiendelea kuwataka watu kutofanya uhalifu kwani kuendelea kufanya hivyo ni kujiweka katika hatari.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com