Christopher Chiza abwagwa tena mahakamani na mbunge wa CHADEMA

Mahakama ya Rufani nchini imefuta rufaa ya kesi ya Uchaguzi iliyofunguliwa na Christopher Chiza dhidi ya Mbunge wa jimbo la Buyungu wilayani Kakonko, mkoa wa Kigoma kwa tiketi ya chama cha CHADEMA Mh. Bilago Kasuku

Rufaa hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Christopher Kajoro Chiza baada ya kushindwa katika kesi ya msingi katika Mahakama Kuu mwaka jana.
Chiza awali alifungua kesi hiyo kupinga Ubunge wa Bilago kwa madai kuwa uchaguzi wa ubunge uliofanyika Oktoba 25, 2015 haukuwa huru na haki, pia aliwasilisha vielelezo mbalimbali mahakamani hapo vinavyoonesha jinsi matokeo ya ubunge yalivyotawaliwa na rushwa, uonevu kwa wananchi na wapiga kura tangu kipindi cha kampeni hadi siku ya uchaguzi.
Afisa habari wa CHADEMA, Tumaini Makene amesema ushindi huo wa leo ni mwanzo mzuri kuelekea katika kesi nyingine ya rufaa dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu kumvua Ubunge Mbunge wa Longido
“Kwa ushindi huu wa leo imebaki sasa rufaa yetu dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu kumvua ubunge Mbunge wetu wa Longido, Mh. Onesmo Ole Nangole. Rufaa yake itasikilizwa Jumatatu ijayo tarehe 14 Agosti 2017 jijini Dar es Salaam” alisema Tumaini Makene.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com