CHADEMA "Yaamsha dude" lingine kwa kaimu Jaji Mkuu


Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA imemuandikia barua Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, kumlalamikia kitendo cha Mahakama nchini kuwanyima dhamana viongozi na wanachama wake pindi wanapofikishwa Mahakamani.

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Prof. Abdallah Safari wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari na kusema wameandika barua hiyo kama azimio ya Kamati Kuu yao kumpa taarifa Jaji Mkuu aviangalie vitendo hivyo wanavyofanyiwa ili visiweze kuendelea.

"Katika barua tuliyomuandikia Kaimu Jaji Mkuu tumeainisha kesi tano ambazo ni mfano wa ukiukwaji mkubwa wa Mahakama katika kuwakatalia dhamana viongozi na wachama wetu ambapo tumemtaka Kaimu Jaji Mkuu kuingilia suala hilo ikiwezekana kukomesha vitendo vya baadhi ya Mahakimu kunyima haki ya dhamana", alisema Prof. Safari.

Aidha, Prof. Safari ameendelea kwa kusema kuwa makosa yote ambayo washtakiwa wanakabiriana nayo yanastahili dhamana kwa mujibu wa Katiba, sheria za nchi na miongozo ya Mahakama za juu.

Pamoja na hayo, Prof. Safari amesema sasa imekuwa mtindo kwa baadhi ya Mahakimu kuwakatalia dhamana watuhumiwa au kuwawawekea masharti magumu licha ya watuhumiwa wengine kuwa na nyazfa kubwa ambayo hawataweza kushindwa kuhudhuria Mahakamani.

"Hivi sasa magereza yamefulika mahabusu ambao wangeweza kudhaminiwa kwa masharti ambayo wasingeshindwa kuyatimiza" amesisitiza Prof. Safari.

Kwa upande mwingine, Prof. Safari amedai dhamana siyo adhabu kama watu wanavyofikilia bali ni kuhakikisha mtu anafika Mahakamani.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com