Baraza La Madiwani Lamfuta Kazi Mhandisi wa Maji Wilaya

Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita limeridhia kumfukuza kazi mhandisi wa maji katika halmashaauri hiyo Rahel Antone kutokana na kushutumiwa kushindwa kusimamia mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria katika kijiji cha Chankorogo.
Pia, baraza hilo limemrudisha kazini Afisa manunuzi wa Halmashauri hiyo, Denice Misaba ambaye naye alikuwa amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma hizo baada ya uchunguzi kubaini hana hatia.
 Akizungumzia hatua hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Elisha Lupunga amesema hatua hiyo ni kufuatia Mkutano wa kamati ya Nidhamu ya baraza la Madiwani baada ya kamati ya uchunguzi wa tuhuma hizo kukamilisha kazi yake. 
Naye Mbunge wa Jimbo la Geita, Joseph Msukuma ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita amesema kutokana na  hasara iliyopata Halmashauri hiyo inatakiwa mhandisi huyo kufidia hasara hiyo ili mradi huo ukamilike kwa wakati.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri hiyo ambao ni wajumbe baraza hilo waliosimama kidete katika sakata la kumvua madaraka mhandisi huyo wanasema kushindwa kwake kusimamia mradi huo umeleta usumbufu kwa wananchi.
Mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2013 na matarajio yake ilikuwa ukamilike mwaka 2015 lakini kutokana na udhaifu wa kiutendaji wa Mhandisi huo umeshindwa kukamilika kwa wakati baada ya kununuliwa vifaa chini ya kiwango na hivyo kushindwa kufanya kazi huku wananchi wakikabiliwa na uhaba wa maji.
 Na Veronica Martine, Geita


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com