AUDIO: Rais Magufuli "Nilipanga Kuivunja Manispaa ya Tanga"

RAIS Dkt John Magufuli amesema alikuwa amepanga kutumia sheria ya TAMISEMI kuivunja Manispaa ya Tanga muda mchache kabla hawajashtuka

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Mkoani Tanga wakati akifungua kiwanda cha kutengeneza saruji cha Kilimanjaro kilichopo mkoani Tanga ambapo amesema kutokana na migogoro iliyokuwepo katika manispaa hiyo iliyosababishwa na baadhi ya wanasiasa, alikuwa amepanga kumtuma waziri wa Tamisemi aje Kuivunja Manispaa hiyo

"Nilikuwa nimepanga kuja kuivunja Manispaa hiyo sasa muda mchache kabla sijafanya hivyo mkaingia kwenye kikao mkakubaliana mkatoa tofauti zenu, sasa sijui ni nani aliwatonya yaani mnabahati sana" amesema Rais Magufuli

Bonyeza Play Hapo chini uweze kumsikiliza:-

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com