AUDIO: Olesendeka atoa Maagizo Mazito Makete, Yamo ya Kuwastopisha watumishi 10

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka ameagiza watumishi wote wanaotuhumiwa kufanya ubadhilifu wa Milioni 120 katika halmashauri ya Makete ambao bado wapo kazini wasimamishwe mara moja

Pia Mkuu huyo wa mkoa ameagiza watumishi wanaotuhumiwa ambao wamehamishwa warudishwe Makete na wengine walioacha kazi wasakwe na warudishwe kujibu tuhuma zinazowakabili

Akizungumza kwenye baraza maalum la madiwani leo lililokuwa likijadili hoja za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali zilizoonesha kuwa halmashauri ya wilaya ya Makete imepata hati ya Mashaka, Mkuu huyo amesema hakuna mtumishi hata mmoja aliyejihusisha na ubadhilifu wa fedha hizo za maendeleo atakayepona


Mbali na hilo Mkuu huyo wa mkoa amesisitiza kuwepo kwa mahusiano mazuri baina ya watendaji wa halmashauri na waheshimiwa madiwani kwa kuwa ushirikiano wao utaepusha changamoto mbalimbali zinazoikabili halmashauri ya wilaya ya Makete kwa sasa

Bonyeza hapo chini usikilize ripoti hii kama ilivyoripotiwa na kituo cha Redio Green FM 91.5:-


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com