UVCCM: Rais Magufuli anamvutia kila Mtanzania

Kaimu Katibu Mkuu (UVCCM) Taifa, Shaka Hamdu Shaka amefunguka na kusema utendaji wa miaka miwili wa Rais John Pombe Magufuli, umemvutia kila Mtanzania na umeibua mjadala Afrika na duniani kote.

Shaka Hamdu alisema hayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya kauli aliyotoa Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi siku kadhaa zilizopita ambapo alidai kama kusingekuwa na Katiba angependelea kuona Rais Magufuli anaendelea kuongoza nchi hata baada ya 2020, kutokana na namna anavyoendesha nchi vizuri na kufanya mambo ya maendeleo.

"Maoni ya mzee Mwinyi bila shaka yoyote yamekwenda moja kwa moja kutokana na kuvutiwa na uchapakazi wa Rais John Pombe Magufuli lakini maoni hayo hayakuwa maamuzi ya mtu wala kushurutishwa na mtu bali ni mawazo yake kama Mtanzania au kama mwananchi, katika jambo la kushangaza mtazamo wa mzee Mwinyi umeshikiliwa bango na kupotoshwa na watu wasiolitakia mema taifa hili. Alichosema au kushauri mzee wetu ni jambo lenye mantiki kulingana na mtazamo wake ambo ulijiegemeza baada ya kuangalia uzalendo wa Rais Magufuli" alisisitiza Shaka Hamdu

Mbali na hilo Kaimu Katibu Mkuu (UVCCM) alisema kutokana na utendaji wa Rais Magufuli na umakini wake kwa watu anaowaongoza umefanya kila Mtanzania kuvutiwa naye na ametikisa dunia katika mijadala.

"Sasa yapata miaka miwili lakini utendaji wa serikali yake ya awamu ya tano licha ya kumvutia kila Mtanzania, umetikisa na kuamsha mijadala nchini, Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na duniani kwa ujumla, mjadala kuhusu utendaji wa Rais Magufuli umetawala kwenye vichwa vya magazeti ya ndani, vipindi vya luninga, na mitandao ya kijamii kitaifa na kimataifa" alisema Shaka Hamdu
Rais Magufuli toka ameingia madarakani mpaka sasa amekuwa gumzo katika mambo mbalimbali likiwepo kutumbua viongozi wazembe, wabadhilifu, kubana matumizi serikalini, na kuleta nidhamu ya kazi miongoni mwa watumishi wa serikali.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com