Ufafanuzi Kuhusu Kampeni ya Magufuli Baki

Kumekuwepo na mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu kampeni mpya ya MAGUFULI BAKI kwa watu wengi kuihusisha kampeni hiyo kuwa ina lengo la kutaka Rais Magufuli abaki madarakani hata baada ya muda wake kuisha.
MO Dewji Blog imezungumza na mwanzilishi wa kampeni hiyo, Laurence Mabawa kutaka kujua kama ni kweli kampeni hiyo ina lengo la Rais Magufuli abaki madarakani hata baada ya kipindi chake cha kuwa madarakani kuisha.
Mabawa amesema jambo hilo halina ukweli wowote na kuwa kampeni hiyo lengo lake pekee ni kumwomba Rais Magufuli aendelee kuwa na msimamo wa kuwatetea wananchi na kuwachukulia hatua watu wote ambao watabainika kutumia rasilimali za nchi vibaya.
“Watu wanapotosha hawaoni ukweli, mimi nimekuja na kampeni hii kumtia moyo Rais Magufuli kumwambia endelee hivyo hivyo na siku zote vitu  vizuri ndiyo husemwa vibaya, hao watu ambao wanapinga hili swala la Magufuli kufanya kazi kubwa hivi ni Watanzania kweli hawa?,
“Sababu kubwa ya mimi kuanzisha Magufuli Baki ni abaki na msimamo wa kuwatetea masikini na rasimili za nchi hii, Tanzania imewahi kuwa na viongozi wengi na sasa ameibuka kiongozi mpya ambaye ameishangaza dunia ambaye ni Rais Magufuli, amefanya kazi kubwa na anaendelea kupambana,” amesema Mabawa na kuongeza.
Aidha Mabawa amesema amepanga kukutana na waandishi wa habari na hapo ndipo atazungumza mambo mengi ambayo yamejitokeza tangu alipozindua kampeni hiyo Julai, 17.
“Hivi karibuni nitafanya mkutano mkubwa na wanahabari kulizungumzia hilo kuwa watu waache upotoshaji na kuzungumza mengine makubwa na nitawaeleza baadhi ya wanasiasa na wanachama wao kuwa waache kutumia vibaya ibara ya 18 ya Katiba ya Tanzania kwa kutoa maoni ya kutukana, wanaitukana serikali, jambo ambalo sisi Watanzania wazalendo hatukubali,
“Pia nitazungumza kuhusu mimi baada ya kutoa tamko la kampeni hiyo kwamba nimesurukika kutekwa na nini kilitokea,” amesema Mabawa wakati akizungumza na MO Dewji Blog.

Chanzo: MO Dewji Blog.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com