Tundu Lissu agoma kutoka mahakamani

Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu amegoma kutoka katika chumba cha mahakama ya wilaya ya Dodoma alipokuwa akifanya shughuli zake za uwakili akihofia kukamatwa na jeshi la polisi  kwa makosa ya uchochezi.

Mwanasiasa huyo ambaye pia ni rais wa chama cha mawakili Tanzania anasema amefikia uamuzi huo baada ya kubaini njama za polisi za kumkamata ambapo anadai awali askari wa jeshi hilo walifika nyumbani kwake Dar es Salaam na kumkosa na baada ya kuambiwa yuko Dodoma wamefika katika viwanja vya mahakama wakisubiri amalize shughuli zake na kisha wamkamate.

Aidha Mhe. Lissu amelitaka jeshi la polisi na baadhi ya viongozi wa serikali kuacha kukamata wanachama na wafuasi wa vyama vya upinzani ambao wanafanya mikutano ya ndani ya yenye lengo la kuimarisha vyama vyao kwani huku kufanya hivyo ni kukiuka demokrasia.

Mpaka ITV inaondoka mahakamani hapo majira ya saa kumi na nusu ambapo shughuli za mahakama zilikuwa zimemalizika Mhe. Lisuu alikuwa bado amesalia ndani ya chumba cha mahakama akiwa na baadhi ya wateja wake


chanzo: ITV


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com