Tundu Lissu achekelea baada ya Mteja wake Kuachiwa Huru na Mahakama

KISUTU: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi na kumwachilia huru Jovenary Shirima ambaye ni mwanafunzi wa Chuo mjini Arusha aliyekamatwa tangu mwezi Januari mwaka huu akituhumiwa kwa makosa ya mtandao, wakili wake Tundu Lissu amenena.

Akizungumza mara baada ya kuachiliwa huru, wakili wa Shirima ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema tangu hiyo kesi ifunguliwe upande wa walalamikaji hawakuweza kuendelea kuhudhuria mahakamani jambo lililopelekea kufutwa kwa kesi hiyo.

“Walalamikaji wameikacha kesi kama walivyokacha walalamikaji wa kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema”.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com