"Tulibaki kuuzwa sisi" - Magufuli

Rais John Pombe Magufuli amesema kuwa Tanzania ilikuwa imebaki wananchi tu kuuzwa kwani baadhi ya viongozi walikuwa hawana uzalendo na walikuwa hawajali rasilimali za nchi bali walikuwa wanaangalia maslahi yao binafsi.

Rais Magufuli amezungumza hayo alipokuwa akizindua mradi wa maji Sengerema, na kudai kuwa wapo viongozi waliokuwa tayari kuuza maisha ya watanzania hata kwa kupewa gari ndogo tu. 
"Mtu alikuwa yuko radhi kuuza maisha ya watanzania kwa Pick-Up, anaachia kila kitu, yaani tumefanya mikataba ya hovyo. Tanzania tumebinafsisha viwanda vyetu vingi, siwalaumu viongozi waliofanya hivyo ila sizuiliwi kuongea ukweli huu, yaani tulibaki kuuzwa sisi. Kuna viwanda vingine vipo Morogoro pale watu wanafugia mbuzi", alisema Rais Magufuli 
Mbali na hilo Rais Magufuli ameutaka uongozi wa Mwanza kufanya uchunguzi juu ya upotevu wa fedha zaidi ya bilioni mbili za maji, na kuwataka watu waliohusika kuiba fedha hizo waanze kuzirudisha wenyewe kabla ya uchunguzi huo kufanyika. 
Rais Magufuli yupo ziarani kikazi jijini Mwanza kwa siku mbili


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com