Taarifa ya Efm Juu ya kifo cha Bikira wa Kisukuma

Marehemu Seth Katende – maarufu kama Bikira wa Kisukuma enzi akifanya kazi EFM.

Kwa majonzi makubwa, Uongozi na wafanyakazi wote  wa Efm Radio na TV-E , unasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzetu Seth Katende – maarufu kama Bikira wa Kisukuma kilichotokea Julai 9 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kutoka kushoto marehemu Seth Katende akiwa na timu nzima ya kipindi cha ubaoni alichokua akitangaza.

Ni vigumu sana kuamini na kukubali msiba huu mzito kwetu lakini kwa kuwa sisi ni binadamu na kila nafsi lazima ionje umauti, tunamuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu mpendwa wetu Seth Katende mahali pema peponi. Amina.
Uongozi na wafanyakazi wa Efm Radio na TV-E unatoa pole kwa familia ya marehemu na wasikilizaji wetu wote walioguswa na msiba huu.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa;  jina lake lihimidiwe.  Amina.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com