T Shirts za Kampeni ya Magufuli Baki Hizi Hapa

Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu ilipoanzishwa kampeni ya Baki Magufuli ikiwa na maana ya Magufuli Baki na Msimamo, waandaji wa kampeni hiyo wamezindua fulana zitakazotumika kwenye kampeni hiyo.
Akizungumza na MO Dewji Blog, mwanzilishi wa kampeni ya Magufuli Baki, Laurence Mabawa amesema kampeni hiyo ina ina lengo la kuunga mkono jitihada ambazo zinafanywa na Rais Magufuli na fulana hizo zitatumiwa na wananchi ambao wanaunga mkono kampeni hiyo.
“Magufuli Baki inatokana na msimamo wake, ni kampeni ya kumtia moyo Mhe Rais na itafanyika nchini nzima, kila Mtanzania popote alipo anatakiwa kumuunga mkono Mhe Rais kwa shughuli zote anazozifanya kwa sababu manufaa yake ni kwa kizazi na kizazi,
“Nimezitundua fulana ambazo zitatumiwa na watu ambao wanamuunga mkono Rais Magufuli, fulana hizi zitakuwa zinauzwa na zinapatikana katika ukubwa wa aina tofauti tofauti, bei itakuwa 22,000 kwa kila fulana na kwa mtu ambaye atahitaji anaweza kuwasiliana na sisi kwa namba +255693 300 704,” amesema Mabawa.
 Mwonekano wa fulana za kampeni Magufuli Baki.
Chanzo: DewjiBlog

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com