Rais Magufuli awapa Wamiliki wa vituo vya mafuta siku 14

Rais John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya vyote mafuta nchini, kuhakikisha wanaweka na kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD) na atakayekiuka agizo hilo atafutiwa leseni ya biashara yake.

Mhe. Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi leo katika ufunguzi wa barabara ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa KM 154 huku akiwataka mawaziri wenye dhamana kuhakikisha wanafuatilia maagizo hayo kuanzia sasa.

"Wanaolalamika kukosa mafuta waendelee kufanya hivyo, ni mara mia tukose mafuta kuliko kuwa na wafanyabiashara wanaokwepa kodi", amesema Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amepiga marufuku wananchi kutozwa kodi kwa mzigo wenye uzito wa tani moja anapousafirisha kutoka wilaya moja kwenda nyingine.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com