Ngeleja ayarudisha Mamilioni ya Escrow aliyopewa na Rugemalila


Mbunge wa Sengerema kwa tiketi ya CCM, William Ngeleja amerudisha pesa kiasi cha Tsh milioni 40.4 alizohusishwa nazo kwenye sakata la Tegeta Escrow. 

Pesa hizo inadaiwa kuwa alipewa mgao yeye na baadhi ya wabunge pamoja na viongozi wengine wa serikali, dini na majaji kutoka kwa James Rugemalila wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd. 

Taarifa ya kurudisha fedha hizo ameitoa leo mbele ya waandishi wa habari ambapo alisema lengo la kuzirudisha ni kuhusishwa kwake na kashfa kuchotwa kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Ngeleja amedai kuwa fedha hizo alipewa msaada kama ilivyokuwa wabunge wengine waliogawiwa na James Rugemalila kwa ajili ya maendeleo ya jimbo lake la Sengerema na kusema licha ya kuwa fedha hizo zilikatwa kodi, ila amerejesha zote.

Hivi karibuni, TAKUKURU iliwafikisha mahakamni Kisutu, Harbinder Singh Sethi na James Rugemalila kwa makosa ya uhujumu uchumi.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com