Mwanamke mbaroni kwa Kumuua Mumewe na watoto wanne

UKIWA bado unadhania kuwa kero la wanandoa kudhulumiana ni kero tu lililoshamiri Kenya na pia kuwa visa vya mmoja katika ndoa kuwaua watoto wake
kikatili ni suala la Kenya pekee, hata Marekani yanatokea.
Kwa sasa, mwanamke mmoja wa Marekani ametiwa mbaroni katika taifa hilo baada ya kudaiwa kuwa mshukiwa mkuu katika mauaji ya bwanake na watoto wao wanne kwa kuwadunga visu.

Habari za idara ya polisi Marekani zinasema kuwa mauti hayo yalitekelezwa Alhamisi asubuhi.
Isabel Martinez, 33, ameshtakiwa kwa makosa matano ya kutekeleza mauaji, kuua kwa ukatili na pia kutumia mabavu katika udungaji huo wa visu katika miili ya waathiriwa hao.
Idara hiyo inasema kuwa baada ya kutekeleza ukatili huo, mwanamke huyo alipiga simu ya dharura ya 911 kujitambulisha.
Habari hizo zinasema kuwa mwanamke huyo kwa sasa amezuliwa katika rumande ya ya Gwinnett.
Habari hizo zinafahamisha kuwa maafisa wa kiusalama wa Gwinnett walipokea simu ya mshukiwa huyo wa kike mwendo wa saa 4:47 ambapo ilionekana kupigwa kutoka eneo la Emory, Loganville.
“Hakuna shaka kuwa Martinez, na ambaye ndiye mshukiwa ndiye alipiga simu hiyo kwetu akitufahamisha kuhusu mauaji hayo,” zasema ripoti hizo.
Wakati maafisa hao walikimbia kuthibitisha madai hayo, wanaripoti kuwa walipata mtoto wa tano akiwa na majeraha mabaya mwilini kando na miili ya watano hao waliokuwa marehemu.
Maafisa hao wanaripoti kuwa wote wa watoto hao walikuwa wa chini ya umri wa miaka 10 huku baba yao akiwa wa miaka 35.
Msemaji wa polisi wa Gwinnet, Koplo Michele Pihera ametoa taarifa akisema, “Kile ambacho husukuma mzazi kutekeleza mauti kwa kiwango hiki kwa watoto ambao amewazaa na kisha kuua mshirika wa uzazi wa watoto hao kwa njia ya kikatili kiwango hiki ni suala ambalo halieleweki.”
Alisema kuwa kitendo hicho ni “uhaini mkuu sio tu kwa waathiriwa bali pia kwa familia yake, familia pana, jamii na taifa kwa ujumla.”


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com