Mume aliyekimbia arudi na kusema "nimemuua mke wangu kwa kumkata kichwa"

MAAFISA wa Polisi katika eneo la Gatundu Kusini walipigwa na butwaa kumpokea mwanamume aliyejisalimisha Alhamisi na akakiri "nimemuua mke kwa kumkata kichwa".
Kwa mujibu wa Mkuu wa polisi wa eneo hilo, Bernard Muli, mwanamume huyo alikuwa ameachiliwa kutoka jela miezi minane iliyopita baada ya kumaliza kifungo cha miaka minne ya kuua bila kukusudia, ambapo alikuwa amemuua mke wa kwanza.

Baada ya kuachiliwa kutoka jela, mwanamume huyo alirejea nyumbani kwao katika kijiji cha Gititu na ambapo amekuwa akiishi na mke wake wa pili ambaye walioana miezi sita iliyopita.
“Sasa amemuua mke huyo na kwa sasa ni wazi kuwa ameua wake wake wawili… Ni suala la kusikitisha kuwa hata kufungwa kwake gerezani hakukumwadilisha kamwe,” akasema Muli.
Muli ameambia Swahilihub: “Mwanamume huyo kwa sasa anazuiliwa na maafisa wa polisi akisaidia katika uchunguzi wa kumwandalia mashtaka mapya ya mauaji, yakihusu mke mwingine wake sasa.”
Akasema: “Inaonekana waziwazi kuwa huyu sio mwanamume wa kukaa na mke. Utamuuaje mke wako wa kwanza, ukioa tena umuue hata huyo?
Inaonekana bongo la huyu mtu sio timamu vile na kwa wakati huu tuko makini sana kuandaa mashtalka dhidi yake kwa kuwa hatungependa arejee katika jamii akiwa na mtazamo huo wake wa kikatili dhidi ya wanawake wanaojitambulisha kama bibi kwake.”
Muli alisema kuwa mwanamume huyo alijitokeza katika kituoi cha polisi akionekana kutulia na akakiri waziwazi amejisafilisha ili aanze mkondo mpya wa maisha gerezani baada ya kutekeleza mauaji.
“Ni suala nyeti hili na sijui ni nini kinachomsumbua mwanamume huyu. Katika umri wake wa miaka 58, anafaa kuwa amekomaa kiasi kwamba anaweza akajifundisha kutokana na makosa yake ya awali. Haonekani kujuta kuhusu lolote ndani ya maisha yake ya hadi sasa na akikiri kuua, utafikiria anakuomba kikombe cha chai,” akasema Muli.
Hata hivyo, alisema kuwa kazi ya maafisa wa polisi ni kutekeleza haki bila ubaguzi na “kwa sasa tutawajibikia kumwandalia mashtaka ya mauaji akikusudia na tuhakikishe tumeandamana na ushahidi mahakamani kuwa ni kawaida yake kuwaua wanawake wanaohusiana naye kimapenzi.”


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com