Mimi kufukuza Makandarasi ni kama kunywa chai – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa yeye kufukuza Makandarasi wanaoachelewa kufanya kazi ni kama kunywa chai huku akisema alipokuwa Waziri alikuwa anawafukuza tu.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati anahutubia wananchi katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Kibondo-Nyakanazi yenye KM 50.
“Muheshimiwa Waziri amezungumza kuhusu barabara kwamba Kandarasi anaenda polepole natoa maagizo kwa Kandarasi . Natoa maagizo kwa Makandarasi na kwa bahati nzuri mimi kufukuza Makandarasi ni kama kunywa chai, sasa asije akanirudisha kule niliko kuwa kwasababu sasa ni baba wa wote kwasababu nilipokuwa mimi Waziri nilikuwa nafukuza tu kwakupitia bodi ya Makandarasi nilikuwa nafuta Makandarasi,” amesema Rais Magufuli.
“Nakuomba Profesa Mbarawa usiwe mpole Makandarasi watakao wanafanya kazi polepole chukua action ili kusudi kama anashindwa kufanya kazi ya ukandarasi akafanye kazi nyingine hata ya kuvua samaki.”


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com