Mikosi tena kwa Halima Mdee, Spika Ndugai aagiza Aitwe Ahojiwe Bungeni

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, ameagiza Mbunge wa Kawe Halima Mdee aitwe kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge ikiwezekana kwa pingu ili ajibu tuhuma za kutoa kauli za kumdhalilisha Spika.

Ndugai ametoa agizo hilo leo bungeni ambapo amesema licha ya mbunge huyo kuwa anatumikia adhabu ya kusimamishwa vikao vya Bunge vya mikutano mitatu, akifanya kosa lolote, yeye kama Spika ana haki ya kumuita kwa ajili ya kuhojiwa kwenye kamati hiyo.

“Mtakuwa mmeona kwenye mitandao mbalimbali mbunge mwenzetu Halima Mdee ameendeleza ujeuri kwa kutoa maneno mabaya ya kumdhalilisha Spika, na mimi niko tayari kwa shughuli hiyo, Kama mnavyojua, mtu hata kama akiwa magereza atapelekwa mahakamani akiwa huko huko magereza, kwahiyo naelekeza kamati ya maadili kwa wakati unaofaa, mtamuita Halima Mdee popote atakapokuwa, hata kama ikibidi aletwe kwa pingu, mtaniletea nitaisaini…..” amesema Spika Ndugai.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com