Mama aliyetupa Kichanga atoa sababu ya kufanya hivyo

Wakaazi wa shehia ya  “Mzambarau takao”  Wete mkoa wa kaskazini Pemba  juzi walikumbwa na simanzi baada ya kumuokota  mtoto mchanga mwenye jinsi ya kiume na anaekadiriwa kua na umri wa siku tatu kwenye  kichaka akiwa amefungwa kwenye mfuko wa saruji na akiwa bado yuhai.

Juma Hija kombo  mkaazi wa Mzambarau takao alisimulia tukio hilo kwasimanzi akisema kuwa, yeye pamoja na mkewe Moza Kombo majira ya saa mbili asbuhi  walikua shambani kuendelea na kilimo, ghafla walisikia sauti ya mtoto akilia kichakani na walipofika  walimuona mtoto  akiwa ndani ya mfuko wa saruji ndani yake mukiwa na makumbi pamoja na nguo chafu ambazo alizongwa nazo.

“wakati tunaendelea kulima mimi na mke wangu tukasikia sauti ya mtoto kwa ikiliya, tukatafuta hatimae tukaona mfuko wa saruji ambapo tuligundua kuwa sauti ya mtoto huyo ndimo inamotokea, baada ya kuufungua tukamuona mtoto akitokwa na mafunza mdomoni na kituvuni”alisema Kombo.

Kombo aliendelea kueleza, mara baada ya kuona hali hiyo walimchukua mtoto huyo mpaka kwa sheha wa shehia hiyo ndg: Rehema Abdalla Omar ambapo kwa kushirikiana na wanakijiji wengine walimuwahisha katika hospitali ya Wete ili kupatiwa huduma ya kwanza na kuyanusuru maisha yake.

Kwa upande wake Muuguzi wa  wodi ya watoto katika hospitali ya Wete Bahati Ali alikiri kumpokea mtoto wa siku tatu aliyeletwa katika mazingira ya kuokotwa, alisema baada ya kumpokea alimpatia huduma.” alikua na kilo 3.1 na anaonekana kuwa alizaliwa akiwa na afya nzuri ” alisema Ali
Uchunguzi uliyofanywa  na  Dk Hawala  Saleh Mohd  kitengo cha uzazi  hospitali ya wete umethibitisha kuwa mama wa mtoto huyo   Hadia Ali Mbarouk  alionekana kuwa ni mtu aliyejiufungua siku tatu nyuma.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 35 ambae  ni mjane mwenye  watoto watatu mara baada ya kukamatwa alisema kuwa, aliamua kumtelekeza mwanawe  kwakua awali alikemewa sana na mamaake kuwa hataki mtoto wa nje ya ndoa.
Amesema kwa kumuhofia mamaake na aibu kutoka kwa ndugu jamaa na wakaazi wengine wa maeneo hayo  aliamua kumtupa mtoto wake ili kujinusura na janga hilo.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa kaskazini Pemba Mlenge Mohd  Mlenge amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa aliyemtupa mtoto huyo  yupo chini ya uwangalizi wa madaktari  katika hospitali ya wete na mara baada ya hali yake kiafya kuwa nzuri hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Mpaka sasa mtoto yupo katika hopitali ya Wete anaendelea kupatiwa matibabu na afya yake inaendelea kuwa vizuri.

Na: Salmin Juma- Pemba


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com