Majigambo Mengine ya Haji Manara Hii leo

Haji Manara amepost picha ya Mbonde kwenye account yake ya instagram akionekana amevaa jezi ya Simba huku akisaini mkataba.

Chanzo cha kuaminika ndani ya Simba kimethibitisha Mbonde kujiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

“Kweli Mbonde amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar na atakuwepo kwenye kikosi chetu cha msimu ujao.”

www.shaffihdauda.co.tz imemtafuta kocha mkuu wa Mtibwa Sugar Zubery Katwila ili kujua kama anataarifa yoyote kuhusu mchezaji wake kusaini mkataba na Simba kwa ajili ya msimu ujao.

“Mimi sina taarifa rasmi, sijapewa taarifa yoyote kuhusu hilo. Hata mimi nimeona kwenye mitandao na kupigiwa simu na waandishi wakiniuliza kuhusu suala hili,” – Zubery Katwila.

“Hadi sasa bado sina taarifa kutoka kwa klabu kwa hiyo siwezi kukwambia chochote.”

Mbonde alikuwepo kwenye kikosi cha Stars ambacho kimeshiriki michuano ya COSAFA 2017 ambacho kimemaliza katika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo huku Mbonde akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliocheza mechi zote (6) kuanzia hatua ya makundi.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com