Kanisa lajengwa Uwanja wa Nane Nane, Mkuu wa Mkoa ageuka Mbogo

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemuagiza Mkuu wa Wilaya  kuchunguza ubadhirifu wa mali na fedha uliofanyika kwenye mabanda ya maonyesho ya Nanenane.

Pia ,amesema anashangaa kuona ndani ya mabanda hayo kuna watu wanaishi na kusema ipo sababu ya kuhoji uhalali wa watu hao kuishi ndani ya viwanja hivyo vilivyopo Njiro pia makanisa yakiwa ndani ya eneo la mabanda ya maonyesho hayo

Amesema maandalizi ya maonyesho ya nanenane yataandaliwa na ofisi yake kupitia kwa katibu tawala na si Chama cha  Wakulima na Wafugaji Tanzania,(TASO) kama ilivyozoeleka.

"Sababu za kukatazwa kushiriki maonyesho hayo kwa nchi nzima ni kutokana na utendaji kazi wao mbovu na ubadhilifu wa fedha, hivyo tunatekeleza agizo la serikali

" Maaandalizi yanaendelea vizuri na Makamu wa Rais Samia Suluhu atakuja kuzindua maonesho haya,"amesema Gambo

Mkuu wa mkoa wa Manyara John Bendera ,amesema maagizo ya kutoshiriki kwenye maandalizi ya maonyesho kwa TASO ni maagizo ya kiserikali kutokana na chama hicho kushindwa kutenda kazi zao.

Amesema pamoja na agizo hilo,bado wako kwenye mikakati ya kukabidhiana majukumu na chama hicho, hivyo amewataka wananchi wanaotaka kushiriki maonyesho hayo kwenda kulipia mabanda yao kwa katibu tawala.

Mwananchi:JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com