Hili ndio Basi la Singida United walilolitambulisha leo

 Klabu ya Singida United imetambulisha ramsi basi lake jipya itakalotumia kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Basi hilo lenye thamani ya Sh 350 milioni limezinduliwa rasmi na litaanza kutumika katika safari za timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu.

Katika basi hiyo, Singida imeweka picha za Rais wa timu hiyo, Mwingulu Nchemba ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani pamoja na picha ya mmiliki wa timu, Yusuf Mwandami.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Festo Sanga alisema wataanza maandalizi yao hivi karibuni ili kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu huku wakitarajia kukamilisha usajili wa nyota wachache waliosalia.

Meneja wa klabu ya Singida United Festo Sanga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kulitambulisha basi lao jipya litakalotumika kwa safari za ndani za timu ya Singida United.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com