Halima Mdee: Sijakoma, Mapambano yanaendelea

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee baada ya kuachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10 kwa kudaiwa kutoa lugha chafu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewashukuru wote waliopaza sauti zao ili haki itendeke kwake huku akisema mapambano bado yanaendelea.

Halima mdee ametumia ukurasa wake wa Tweeter kutweet shukrani hizo huku akisema mapambano yanaendelea.

Mhe. Halima ametweet

Kwa heshima KUBWA niwashukuru sana wote mliopaza sauti zenu kutaka haki itendeke kwangu na kwa watoto wetu wa kike! #Mapambano yanaendelea!
Kwa heshima KUBWA niwashukuru sana wote mliopaza sauti zenu kutaka haki itendeke kwangu na kwa watoto wetu wa kike!  yanaendelea!

Halima Mdee alidaiwa kutoa maneno hayo ya kukashifu na ya uchochezi katika mkutano wake wa Baraza la Wanawake Chadema uliofanyika katika ofisi za baraza hilo wakati akizungumza na wanahabari.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com