Halima Mdee aliamsha Dude la Mbowe....Soma Alichokisema

Mara baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu Victoria Nongwa kumuachia Mbunge Halima Mdee kwa Dhamana ya ahadi ya Shilingi 10 Leo Julai 10, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema wataendelea kuzungumza na kusimamia haki bila kuogopa Polisi na Wakuu wa wilaya.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemsomea shtaka la kutoa lugha ya matusi Mbunge Halima Mdee, ambaye amekana shtaka hilo na kuachiwa kwa dhamana ya Tsh. Milioni 10.

Akisoma shtaka hilo, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo Julai 3, 2017 ambapo Mdee anadaiwa kutoa lugha ya matusi na ya uchochezi huku akitoa kauli ya kwamba rais afungwe breki.


Baada ya kukana shtaka hilo Hakimu alisema mshtakiwa huyo ambaye wakili wake ni Peter Kibatala ana haki ya kupewa dhamana, ndipo akadhaminiwa na madiwani wawili wa Chadema 


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com