Everton wamvuta Kikwete Taifa

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ni moja ya maelfu ya mashabiki waliohudhuria uwanja wa Taifa kushuhudia mechi kati ya Everton na Gor Mahia.
Rais Mstaafu Dkt Kikwete wa pili kwenye picha
Dkt Kikwete hakuwa peke yake pia aliongozana na Rais Mwenzie Mstaafu wa awamu ya Pili Mhe. Alhaji Hasani Mwinyi.
Leo nimeungana na wananchi wenzangu kuangalia mechi ya Everton na Go Mahia.“ameandika Mhe Kikwete kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Kwenye mchezo huo Everton wameigaragaza Gor Mahia kwa goli 2-1, Magoli ya Everton yamefungwa na Wayne Rooney na Kieran Dowell huku goli pekee la kufuta machozi la Gor Mahia likitundikwa kimyani na Tuyisenge Jacquer.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com