Ebitoke: Mi na Ben Paul Bado Hatujafungua Mlango

Ebitoke

Msanii wa vichekesho Ebitoke amefunguka na kusema Ben Pol mpaka dakika hii bado hajafanikiwa kufungua mlango wa binti huyo hivyo anadai mpaka sasa bado hajawahi kulala na mwanaume yoyote yule katika maisha yake. 

Ebitoke amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana EATV na kudai Ben Pol bado hajafanikiwa kumuondoa bikra.

Ben Pol na Ebitoke wanadaiwa kuwa ni wapenzi wenye malengo ya mbali ikiwa ni pamoja na kupeana support katika kazi zao za sanaa, ingawa wapo baadhi ya watu ambao wanaona kama watu hao wanafanya maigizo na mapenzi yao kuonekana kama njia ya kujitangaza na kuzidi kupata kiki katika kazi zao, ingawa kwa Ben Pol siku ya Jumamosi alikiri kuwa kwa mara ya kwanza kukutana na Ebitoke walikutana Bahari beach na kuzungumza mambo mengi zaidi ya mapenzi yao.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com