CHADEMA Watishia Kuandamana....Polisi Watoa ONYO

Baraza la  Vijana la Chadema(Bavicha), wamesema wanatarajia kufanya maandamano ya amani yenye lengo la kuipongeza kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Akizungumza leo Jumatatu katika mahafali ya Umoja wa Wanachama wa Chadema Vyuo Vikuu (CHASO), Mkoa wa Kilimanjaro, Katibu Mwenezi wa Bavicha, Edward Simbeyi alisema kuwa watafanya maandamano mapema mwa mwezi huu ili kuipongeza kambi hiyo ambapo amesema imekuwa ikipigania rasilimali za nchi.

Simbeyi ambaye ni mratibu wa CHASO taifa,alisema wanakusudia kufanya hivyo kama chama cha CCM  kilivyofanya maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kuzuia mchanga wa madini (Makinikia).

Alisema kuwa wabunge wa upinzani wamekuwa wakipambana kwa kujenga hoja  bungeni kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zao wenyewe badala ya watu wachache kunufaika.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alisema kuwa maandamano yalishapigwa marufuku na  hayaruhusiwi kufanyika mahali popote.

“Kama walijitokeza watu wakitaka kufanya maandamano ya kumpongeza Rais wakazuiliwa na wao pia wasijaribu kufanya hivyo,”alisema Issah.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com