Bifu la Tanzania na Kenya lamalizika Leo

Mkutano umeandaliwa kati ya Tanzania na Kenya kuondoa marufuku iliyokuwepo ya uingizwaji wa bidhaa zinazoingia katika mataifa hayo mawili kutoka pande zote mbili.
Bendera ya Tanzania na Kenya pamoja
Waziri wa maswala ya kigeni na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga alitangaza kuwepo kwa uamuzi huo kufuatia majadiliano kati ya rais John Pombe Magufuli wa Tanzania na Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Kwa muda mrefu mataifa  haya hayakuwa na mahusiano mazuri ya kibiashara kwa kuwekeana marufuku ya bidhaa kutoka Tanzania kuingia Kenya ilitokana na wasiwasi wa kiusalama na ubora wa bidhaa huku Tanzania ikijibu kwa kuweka marufuku kwa bidhaa za Kenya kama vile matairi ya gari, mafuta ya kupaka mkate na maziwa.
Katibu wa viwanda na uwekezaji nchini Tanzania Adolf Mkenda awali alisema hakuna hatua zilizochukuliwa kutoka Nairobi tangu mwezi Februari na Juni wakati mataifa hayo mawili yalipokubaliana kwamba marufuku hizo ziondolewe.
Wahida Mbaya.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com