Bendera za CHADEMA zamponza mbunge wa Mbozi

Mbunge wa Mbozi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Pascal Haonga ameitwa na Jeshi la Polisi kutokana na bendera za chama chake kupepea kwa wingi katika mji wa Mlowo wilayani Mbozi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange alimuita mbunge huyo na kumhoji kutokana na bendera hizo kupeperushwa kwa wingi wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwasili katika eneo hilo ili kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.
Pascal Haonga amesema kuwa alipigiwa simu na kamanda huyo na kutaka waonane Ikulu ndogo ya Mkoa wa Songwe baada ya kuonana walifikia makubaliano ya kutoondoa bendera hizo.
“Miongoni mwa mambo tuliyozungumza ni pamoja na kupandishwa kwa bendera za CHADEMA, katika Mji wa Mlowo, mazungumzo yameisha na hakuna bendera zitakazoshushwa,” alisema Haonga.
Wahida Mbaya.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com