AUDIO: Lupila Kwisha Kazi, Mkuu wa Mkoa wa Njombe amaliza Kila Kitu

 Mkuu wa mkoa wa Njombe Mh Christopher Olesendeka akizungumza na wananchi wa Lupila

Mgogoro wa soko uliodumu kwa miezi kadhaa baina ya wananchi wa kata ya Lupila wilayani Makete mkoani Njombe na viongozi mbalimbali umemalizika baada ya mkuu wa Mkoa hii leo kufanya ziara kijijini hapo

Baadhi ya viongozi wa chama tawala na serikali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy, Diwani wa kata hiyo Mh. Daniel Okoka pamoja na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Langael Akyoo ni miongoni wa waliomuomba mkuu wa mkoa kutolea uamuzi mgogoro huo uliopelekea shughuli za maendeleo kusimama

Imeelezwa kuwa chanzo cha mgogoro huo ni agizo la watendaji wa serikali kufunga biashara za wananchi hao na kuwataka kwenda kufanya biashara zao katika soko lililopo kwenye kata hiyo hali iliyozua mtafaruku kutokana na wananchi wengine kuwa mbali na soko hilo hivyo kupelekea kutembea umbali mrefu kufuata mahitaji

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka ametoa maamuzi yaliyopelekea mgogoro huo kumalizika ambapo ameagiza wananchi hao kufanya biashara kwenye vitongoji vyao kama walivyokuwa wakifanya awali, ilimradi wasivunje sheria na taratibu za nchi

Aidha mkuu huyo wa mkoa ameagiza wananchi hao licha ya kuruhusiwa kuendelea na biashara zao katika maeneo yao lakini wahakikishe wanalipa ushuru kwa kuwa fedha hizo ndizo zinazotumiwa na serikali kwa ajili ya kuwaletea maendeleo

Musa Sanga ni mwananchi wa kijiji cha Lupila amemshukuru mkuu wa Mkoa kwa kufika na kutatua mgogoro huo, na kusema yaliyopita yamekwisha na kwa sasa wanaanza ukurasa mpya wa kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta maendeleo ya kijiji hicho

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amefungua chumba cha upasuaji katika Kituo cha afya Lupila huku akimuagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Makete kupeleka gari kwa ajili ya kituo hicho kutokana na gari lililopo sasa kuharibika
 Mkuu wa mkoa akifungua chumba cha Upasuaji katika kituo cha afya Lupila
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa

Gari la kituo cha afya Lupila likiwa "juu ya Mawe"

Sikiliza taarifa hii kama ilivyoripotiwa na kituo cha redio Green FM kwa kubonyeza alama ya Play hapo chini:-


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com