Ajali ya Gari yaua Songea Ruvuma

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Sultani Yusuph mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa Kibaha mkoa wa Pwani amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa kwa ajali ya gari iliyotokea leo katika kijiji cha Gumbiro kwenye kona za Majimaji wilaya ya Songea mkoani Ruvuma ambapo gari lililobeba makaa ya mawe lenye namba za usajiri T-224 CYV aina ya Howo.

Gari hilo lilikuwa limebeba makaa ya mawe kutoka mgodi wa makaa wa Ngaka uliopo katika wilaya ya Mbinga ambapo walikuwa wanapeleka Kibaha mkoa wa Pwani Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma SACP Gemini Mushy amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari hilo kushindwa kumudu kona,amesema taratibu za kisheria zinafanyika za kumfikisha mahakamani.

Tingo msaidizi wa gari hiyo Shomari Yusuph amesema Dereva Pazi Yusuph alikuwa na mwendo kasi alipofika kwenye mteremko wa kona za majimaji aliondoa gia aliweka Free ili kubana matumizi ya mafuta ndipo ikamshinda kumudu kona ikapinduka,amesema kwenye gari hiyo walikuwa watu watatu ambao ni ndugu wa familia moja majeruhi Pazi Yusuph anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Songea.

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linaendelea kuwaonya madereva wa vyombo vya moto kuwa makini kwenye maeneo yenye kona,miteremko na makazi ya watu


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com