ADC wajitosa kwa Rais Magufuli, waomba abadili msimamo wake

Chama cha ADC  kimemwomba Rais Magufuli katika miaka hii mitatu iliyobaki kubadilisha msimamo wa kuzuia kufanywa kwa   mikutano ya hadhara inayotakiwa kufanywa na vyama vya upinzani.

Akizungumza katika kuelekea maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa  chama hicho  Katibu mkuu wa chama cha ADC , Doyo Hassan Doyo amesema wao wanania nzuri ya kufanya siasa nakusema Rais  asione kwamba vyama vyote vinakauli mbovu katika kufikisha  ujumbe kwa jamii.
Doyo amesema suala la Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa  vyama vingine vya Demokrasia na kusema wao hawana mbunge wala diwani hivyo wana ufinyu mkubwa wa kufanya siasa, na kusema kuwa  wao wanapaswa kufanya siasa kwa nguvu zote ili kuongeza wananchama na hatimae kujipatia viti vingi vya uongozi.

"leo umezuiwa kusema inamaana hutoweza kupata sapoti ya watu  na watu hawatoweza kufahamu sera za chama chako kutokana kutoweza kufanya mikutano ya kisiasa" Alisema Doyo. 

Aidha Chama hicho kinafanya maadhimisho hayo kwa njia ya ziara ambapo watatembelea baadhi ya taasisi za kidini,magereza ,hospitali,pamoja na vyombo vya habari.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com