Zaidi ya magari 300 yamekwama Wilayani Mkuranga mkoani Pwani

Zaidi ya magari 300 yamekwama katika eneo la njia panda ya kisele Kiparanganda,Wilayani Mkuranga mkoani pwani, kufuatia lori na tela lake kuanguka na kusababisha maelfu ya abiria kutoka mikoa mbalimbali nchini kusota kwa zaidi ya saa 24 , kabla ya kupata msaada wa kusogeza lori hilo lililoziba barabara.
Kufuatia lori lenye Namba za usajili T 782 ALR lililokuwa likivuta tela kupata ajali katika eneo hilo na kuacha nafasi ndogo na kusababisha lori lingine lenye usajili T 356 DFH lililobeba shehena ya saruji kuziba njia iliyobaki kumesababisha mabasi ya abiria na malori mengine yaliyobeba mizigo katika barabara hiyo iendayo mikoa ya pwani,lindi,Mtwara,Ruvuma pamoja na Nchi jirani ya Msumbiji kutopita , na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.
Baadhi ya wananchi waliopatwa na kadhia hiyo na kukutwa na channel ten katika eneo hilo pamoja na kuhangaikia magari yao kuweza kupita walikuwa na haya ya kusema ikiwemo ombi kwa serikali.
Changamoto kama hizo zinatokea mara kwa mara katika barabara hiyo kutokana na maeneo mengi kukosekana kwa maeneo ya dharura ya kutengeneza barabara ya dharura huku mitambo ya kuinua vitu vizito ikilazimika kutoka jijini Dar es salaam


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com