Yule Mtu Aliyeuawa na Polisi kwa Ujambazi… Ndugu Washusha Kisomo Kizito

Ndugu wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Salum Almas (pichani) aliyeuawa na polisi maeneo ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar akidaiwa ni jambazi, wamedai kusoma kisomo kizito kwa ajili ya wale waliosababisha kifo cha ndugu yao huyo.

Akizungumza na Gazeti la Amani, mjomba wa Almas, Tullehya Abdulrahman amekiri kusoma kisomo hicho akieleza kuwa, wamefanya hivyo kwa kuwa wanaamini ndugu yao hakuwa jambazi.

“Ni kweli kama ndugu tumesoma kisomo kwa sababu tunaamini ndugu yetu Almas aliuawa kimakosa na jeshi la polisi na siyo kweli kwamba alikuwa jambazi kama ambavyo mamlaka ilisema.

“Siku zote malipo ni hapahapa duniani na tunaamini kilio chetu Mungu atakisikia. Doa la ujambazi ni mzigo kwetu, lakini hata hivyo kuna kesi mahakamani juu ya ndugu yetu na inatarajiwa kutajwa Julai 14 mwaka huu,” alisema.

Ikumbukwe kuwa, kifo cha Almas kilizua utata mkubwa kiasi cha ndugu wa marehemu kususia kumzika ndugu yao huku wakitaka jeshi la polisi likiri kuwa lilimuua kimakosa.

Ni takriban majuma kadhaa sasa yamepita tangu Almas kuuawa na bado mwili wake uko mochwari kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.

STORI: BONIPHACE NGUMIJE, AMANI


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com