Watuhumiwa 9,140 mbaroni kwa dawa za kulevya

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Masauni amesema Jeshi la polisi lilifanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 9140 wa dawa za kulevya ambapo watuhumiwa 14,410 kesi zao zinaendelea Mahakamani na zipo katika hatua mbalimbali kuanzia Oktoba 2015 hadi Aprili 17.
Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri Masauni wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum, Zainabu Athuman Katimba lenye sehemu abc lililohoji
(a)Je ni hatua gani zimechukuliwa tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani baada ya kuwabaini na kuwachunguza wale wote waliojihusisha na mtandao wa dawa za kulevya (b) Je serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia vijana wanaojiingiza kwenye dimbwi la dawa za kulevya (c) ni vijana wangapi kwa nchi nzima kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita wamepatiwa tiba kuondokana na dawa za kulevya?
“Takwimu zinaonyesha kati ya Oktoba 2015 hadi Aprili 17, Jeshi la polisi lilifanikiwa kuwakamata jumla ya Watuhumiwa 9140 wa dawa za kulevya ambapo watuhumiwa 14,410 kesi zao zinaendelea Mahakamani na zipo katika hatua mbalimbali,watuhumiwa 2401 walikutwa na hatia,watuhumiwa 615 waliachiwa huru na watuhumiwa wengine 13,071 kesi zao zipo chini ya upelelezi,” alisema Mh. Masauni.
“Jeshi la polisi kwa kupitia programu ya kuzuia uhalifu imeendelea kutoa huduma ya urekebishaji kwa waathirika wa dawa za kulevya kwa kutumia vikundi mbalimbali vya michezo nchini chini ya miradi ya kuzuia uhalifu kama vile familia yangu haina uhalifu,na klabu ya usalama kwetu kwanza. Muheshimiwa spika vijana 3000 walipatiwa tiba katika kipindi cha miaka 10 iliyopita kwa kushirikiana na wadau.”


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com