Wanaswa Kwa Ubakaji wa Mtoto wa Miaka 5

Wanaume wawili, Issa Njunja na mwenzake ambaye jina halikupatikana mara moja, wakazi wa Keko jijini Dar, wanadaiwa kunaswa kwa ubakaji wa mtoto mwenye umri wa miaka mitano (jina linahifadhiwa kwa sababu za kitaaluma) kisha kupandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza kwenye Mahakama ya Wilaya ya Temeke kwa tuhuma hizo.

Wikienda liliwashuhudia washitakiwa hao wakipandishwa kizimbani juzikati ambapo umati uliokuwa mahakamani hapo ulisitisha kufanya shughuli zao na kuanza kuwatolea macho na kuwajadili.

 Njemba hao wanaokabiliwa na kesi hiyo yenye namba CC/129/2017, wanadaiwa kumfanyia ukatili mtoto huyo wakati akitoka shuleni.


Katika kesi hiyo, ilidaiwa kuwa, Njunja alimkamata mtoto huyo alipokuwa akitokea shuleni na kumvutia chumbani kwake huko Keko jijini Dar huku mwenzake huyo akiwa amesimama mlangoni kuangalia usalama.

Washitakiwa hao, wakiwa mahakamani hapo, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Mwakihawa Mwakihawa walikana kutenda kosa hilo hivyo kurejeshwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena.

Wakati washitakiwa hao wakitoka kizimbani, umati ulikuwa ukiwaangalia kwa mshangao na kila mmoja akiongea lake kutokana na tuhuma zenyewe ilihali kwa sasa idadi ya wanawake ni kubwa kuliko wanaume.
  
STORI: MWANDISHI Wa GPL, DAR

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com