Vikundi kutoka Makete Vyazoa TUZO za Uhifadhi wa Mazingira


Katika kutambua jitihada zinazofanywa na wananchi, vikundi, taasisi za kiserikali ,vikundi vya koo vinavyojitolea kutunza MAZINGIRA ilibuniwa Tuzo ya kuhifadhi MAZINGIRA ya TANAPA 2017. 

Tuzo hizo zilihisaniwa na WWF,SPANEST,RWBB, na TANAPA. Ambapo elimu ilitolewa kwa njiani ya redio Kitulo Radiofm, Ebony FM na mikutano ya hadhara.

Elimu ilijikita katika kuwataka wananchi kushiriki kutunza MAZINGIRA .Baada ya kupata elimu wananchi walihamasishwa kujaza fomu ili kuingia katika shindano.Vigezo vya ushiriki vilikuwa kama ifuatavyo.

A.Uhifadhi wa vyanzo vya maji na misitu ya asili
B.Upandaji miti asilia Rafiki kwa maji
C.Uhifadhi wa ardhi
D.Utoaji elimu ya Utunzaji wa mazingira.
E.Uhifadhi wa shoroba /mapito ya wanyamapori

Kwa kuzingatia vigezo hivyo kamati ya Tuzo imeona washindi wafuatao wamekuwa washindi kati ya washiriki 44 waliojitokeza.

1.Kijiji cha Ng'onde-Washindi wa kwanza kwa kuhifadhi vizuri misitu 5 ya asili(Tsh.2,000,0000)
2.Kikundi cha Hifadhi MAZINGIRA Magano -Washindi wa pili wao walipanda miti asili Rafiki kwa maji na kutunza vema vyanzo vya maji 6 ZAWADI Tsh.1,500,000
3.Kijiji cha Kigala - washindi wa Tatu wao wanatunza vizuri vyanzo vya maji na kuhifadhi misitu 4 ZAWADI yako ni Tsh.1,000,000.

ZAWADI zao zimetolewa leo katika kijiji cha Mabadaga Wilaya ya Mbarali na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya aliyekuwa mgeni Rasmi katika siku ya Mazingira duniani iliyoadhimishwa na Wilaya za Kilolo, Mufindi, Wanging'ombe, Makete na Mbarali.

Lengo la Tuzo ni kujaribu kurejesha mtiririko wa Mto Ruaha Mkuu ambapo kiasi chake cha Maji kinapungua.

Ikumbukwe kuwa Tuzo hizi ni endelevu na wakani mashindano yatakuwepo.

Watu mbali mbali waanze kujiandaa kwa mashindano.Image may contain: one or more people, people standing, shoes and outdoorImage may contain: one or more people and outdoorImage may contain: 1 person, outdoorImage may contain: 4 people, people smiling, people standing and outdoorImage may contain: one or more people, people standing and outdoorImage may contain: 2 people, people standing and outdoorImage may contain: one or more people, people standing and outdoor


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com