Songwe: Baadhi ya madereva wakamatwa ,waswekwa rumande

MADEREVA zaidi ya 40 wanaoendesha magari ya abiria aina ya Coster zinazofanya safari kati ya Tunduma – Mbeya,wamakamatwa na jeshi la polisi mkoani Songwe,na kuwekwa rumande,wakituhumiwa kufanya mgomo unaodaiwa kuwa sio rasmi.

Hatua ya madereva hao kufanya mgomo,imekuja baada ya wenzao 4 kukamatwa na jeshi la polisi usalama barabarani na kuwaweka lumande kwa madai kuwa walichukua abiria eneo lisilo rasmi eneo la mwaka halmashauri ya mji wa Tunduma wilayani Momba.

Baada ya kukamatwa madereva hao,kumepelekea chama cha madereva mkoani Songwe kuitisha mgomo,wakishinikiza jeshi hilo kuwaachia huru wenzao kama wanavyoeleza.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com